Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mkusanyiko huo uliwatumia pongezi viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, chini ya uongozi wa Ayatollah Sayyid Ali Khamenei.
Katika ujumbe uliomlenga Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi imeelezwa kuwa: Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu nchini Lebanon unajivunia, kwa kuwadia majira ya kuchipua ya mwaka wa arobaini na saba wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, kuwasilisha salamu bora na pongezi kwa mhimili wako mtukufu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, mapinduzi haya yaendelee kuwa mwanga unaong’aa katika ulimwengu wa Kiislamu, yaoneshe njia ya heshima na utukufu, na yaongoze mhimili wa muqawama hadi ushindi wa mwisho dhidi ya adui Mzayuni, hadi siku ambayo bendera itakabidhiwa kwa Imam Mahdi (a.f).
Mkusanyiko huo umeongeza kuwa unaamini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo inabeba jukumu la msingi, hasa baada ya operesheni “Tufani al-Aqsa”, ambapo ilikabiliwa na mashambulizi makubwa ya kihistoria yaliyoongozwa na Marekani kwa uungwaji mkono wa utawala wa Kizayuni katika mfumo wa vita dhalimu; hata mashirika ya kimataifa hayakuweza kukaa kimya, hadi Mahakama ya Kimataifa ilipolaani tukio hilo kwa sababu ya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Ghaza. Vita hivyo pia viliikumba Lebanon.
Mkusanyiko wa wanazuoni ulisema kuwa, mhimili wa muqawama katika vita hii ulitoa makamanda wake bora zaidi, na wakiogozwa na Hassan Nasrallah, Sayyid wa mashahidi wa umma. Ingawa kujitolea huko kuliacha huzuni kubwa, kuliongeza nguvu na ustahimilivu wao; kama ilivyokuwa kwa Waislamu wa mwanzo baada ya kujeruhiwa katika vita vya Uhud waliposimama tena katika vita vya Hamra’ al-Asad, nao pia walisimama na kupata ushindi uliolazimisha utawala wa Kizayuni kuomba usitishaji vita nchini Lebanon na baadaye Gaza.
Mkusanyiko huo ulisisitiza kuwa ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya adui Mzayuni na Marekani katika vita vya siku kumi na mbili, licha ya kuuawa kishahidi baadhi ya makamanda waandamizi, ni ushahidi wa wazi wa nguvu ya Iran na mhimili wa muqawa.a.
Ujumbe uliendelea kusema kwamba; hali ya sasa ni matokeo ya miaka ya juhudi na jihadi ya Jamhuri ya Kiislamu; jamhuri iliyofikia nafasi hii kwa baraka ya uongozi wa kimungu wa Ruhollah Khomeini, mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na uongozi wa hekima wa Imam Khamenei. Walisema, adui Mzayuni baada ya kushindwa katika mapambano ya “Tufani al-Aqsa” na vita vya siku kumi na mbili na Iran, anajaribu kurejesha nguvu zake kwa kuchochea fitna za kikabila, kidini na kimadhehebu ili kuvunja safu za Umma wa Kiislamu na mhimili wa muqawama.
Mkusanyiko huo ulieleza kuwa; kwa sababu hiyo wanatangaza utayari wao wa kuwa chini ya uongozi wa hekima wa Imam Khamenei ili kukabiliana na fitna hizo na kuzizima tangu mwanzo wake; jambo ambalo linaweza kufikiwa kupitia kueneza uelewa na “jihadi ya kubainisha ukweli” ambayo ameihimiza.
Walisisitiza pia kuwa wana uhakika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaingia katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani kutoka katika msimamo wa nguvu, na haitarudi nyuma kamwe katika maendeleo yake ya nyuklia ya amani, wala haitajadili uwezo wake wa ulinzi.
Mwisho wa ujumbe huo, mkusanyiko huo ulisisitiza kushikamana kwao na uhusiano maalumu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na uaminifu wao kwa Imam Khamenei, huku wakitoa shukrani kwa kuwaunga mkono na kwa waja wema wa Umma, na wakatumaini uhusiano huo uimarike zaidi ili kuleta kheri, maendeleo na ustawi kwa mataifa ya Iran na Lebanon.
“Kwa heshima na salamu nyingi, tafadhali pokokea hisia zetu za mapenzi na shukrani.”
Maoni yako